Announcements

Maelezo kuhusu mfumo wa MSSIS

1. *Kusajili Mitihani ya Ndani (Internal Exams) kwenye mfumo:* Mtaaluma/Makamu/Mkuu watakuwa na access kupitia akaunti zao kusajili mitihani ya ndani kwa kufuata hatua zifuatazo; watabofya `Academics=>Exams=>Register (icon hii iko juu kulia)=>Create exam=>select exam type, chagua internal=>Exam Name, andika jina la aina ya mtihani  mfano; Mtihani wa Muhula wa kwanza/Terminal Exams. *NB* Tusijaze mwezi na mwaka wa mtihani husika, mwezi na mwaka mfumo itajaza automatically baada ya kujaza start na end dates=>Start na end dates, jaza tar ya kuanza na kumaliza mtihani=>Select classes&subjects, chagua madarasa na masomo yanayoshiriki mtihani huo kwa kutick=>Create grades, jaza gredi zitakazotumika kwa mtihani husika kwa kuanza na A, kisha bofya Add grade kujaza B, C.., (kwa sekondari lazima pia tujaze na point ya kila grade k.v. A ina pt 1, B pt 2, C pt 3, D pt 4 na F pt 5) => Create.`

2. *Kusajili watahiniwa wa Mitihani ya ndani na nje (Internal & External exams) kwenye mfumo* Wakuu/makamu/Wataaluma kupitia akaunti zao wanaweza kusajili watahiniwa (Candidates). Baada ya kusajili jina au aina ya mtihani, atasajili watahiniwa sasa kwa kubofya; `Academics=>Exams=>bofya button ya View/jicho ya mtihani husika=> Registered Candidates (Chagua darasa moja moja e.g. Class I/Form I)=>Register Candidates=> Select candidates to register (Chagua watahiniwa wa kusajili) kwa kutick=> Register.` Baada ya ku-register, mfumo unachakata automatically namba za mitihani za watahiniwa wote na kwa hatua hii, kwa sasa wataaluma/wakuu wanaweza kupakua CAL (collective attendance list) ya wanafunzi wote wa darasa husika waliosajiliwa kwa mtihani huo kwa kubofya `Exams=>View Exam=>Registered Candidates=>Download CAL`. Hiyo CAL itaonesha wanafunzi wote waliosajiliwa kwa kila somo, idadi ya masomo kwa kila mwanafunzi aliyosajiliwa kusoma kwa shuleni. *NB:* alama ya dash (-) inaonesha, mwanafunzi husika amesajiliwa kusoma somo husika. *Angalizo;* Kwa wanafunzi waliosajiliwa kwenye mfumo kusoma masomo na unauhakika kuwa kwa mtihani huu, hawatashiriki kwa changamoto mbalimbali, hivyo wasisajiliwe kufanya mtihani ili kuepuka kuwa na orodha ndefu ya wanafunzi ambayo wengine ni watoro wa mda mrefu. Pia, kwa kuwa function ya kusajili watahiniwa itakuwa inategemea 100% wanafunzi waliosajiliwa kwenye mfumo na wanaosoma masomo husika.

3. *Jinsi ya kupakia alama/scores za mitihani kwa kila somo* Kila mwl wa somo aliyesajiliwa kwenye mfumo kupitia akaunti yake, atakuwa na access/uwezo wa kujaza alama na kupakia kwenye mfumo kwa kubofya `Teaching=>Exam results Upload=>chagua aina ya mtihani husika=>bofya Select kitufe kilichopo kulia mwishoni mwa mtihani husika=>Chagua somo ambalo unataka kuingiza matokeo kwa kubofya kitufe cha Select kilichopo kulia pembeni mwa somo husika=>Download template=>fungua mkeka uliopakua wa excel format, jaza alama za watahiniwa wa somo lako=>Save hiyo template=>rudi kwenye mfumo bofya choose file=>chagua hiyo template ya alama ulikoisave=>Upload` *NB:* Kwa mtahiniwa ambaye amesajiliwa na hajafanya mtihani, ASIJAZIWE chochote kwenye cell/kibox chake k.v. O au X, kwa ufupi kisanduku chake kibaki wazi. Pia, mtaaluma/makamu/mkuu watakuwa a access ya kupakia mikeka ya masomo yote kupitia akaunti zao kwa kufuata steps hapo juu.

4. *Jinsi ya kupublish/kutangaza matokeo ya mitihani* Mkuu (kwa mitihani ya ndani) ndo atakuwa na access ya ku-publish matokeo ili yaweze kuonekana kwa akaunti ya staffs wote kwa `kubofya Academics=>Exams=>bofya kwenye kijicho/view button ya mtihani husika=>bofya publish.` *NB:* Matokeo yakishakuwa published, hakutakuwa na fursa ya mwl wa somo yeyote kupandisha/kufanya mabadiliko yeyote ya alama za watahiniwa. Ikitokea kuna haja ya kufanya changes, ajulishwe mkuu wa shule ili Unpublish matokeo ili mwl husika aweze kufanya changes ya scores za watahiniwa.

5. *Jinsi ya Kuview Matokeo ya mtihani ya ndani*  Baada ya matokeo kuwa Published/kutangazwa rasmi na Mkuu wa shule (Mitihani ya ndani), walimu wote kupitia akaunti zao watakuwa na access/uwezo wa  kuangalia na kupakua PDF za Matokeo ya mitihani iliyofanyika kwa kubofya `Academics=>Exams=>bofya kwenye button ya kuview Matokeo ya mtihani husika kilichopo pembeni ya button ya jicho kulia mwa jina la mtihani=>ukurasa wa matokeo ya mtihani husika utaonekana, kisha anza kubofya links za matokeo husika kwa kuchagua darasa moja moja=> unaweza kupakua pia PDF zake kwa kubofya export to PDF button iliyeko upande wa kulia juu mwa page ya kila tathmini ya matokeo.` *NB:* Kwa matokeo ya jumla/wanafunzi unaweza kuview na kupakua kwa mfumo wa kawaida, NECTA format na Order by Position kama yanavyoonekana kwa pages husika kwa select/kutick format unayoihitaji kisha bofya export to PDF.

*_Kwa changamoto yeyote pia simu kwa wataalam wetu_*
1. Pius-Simiyu: 0710231026
2. Vincent-Dodoma: 0759640777
3. Fugo-Dodoma HQ: 0625973343

Related Articles